of 14
All materials on our website are shared by users. If you have any questions about copyright issues, please report us to resolve them. We are always happy to assist you.

Uponyaji wa Mwili. # 26 Healing of the Body

Category:

News & Politics

Publish on:

Views: 111 | Pages: 14

Extension: PDF | Download: 0

Share
Description
166 Uponyaji wa Mwili Utangulizi Kila muumini yapampasa ajibu swali hili: Je uponyaji wa kiroho ni sehemu yangu? Uponyaji wa kiroho ni tendo la Mungu la neema linalofanywa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Transcript
166 Uponyaji wa Mwili Utangulizi Kila muumini yapampasa ajibu swali hili: Je uponyaji wa kiroho ni sehemu yangu? Uponyaji wa kiroho ni tendo la Mungu la neema linalofanywa kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Uponyaji huu unajumuisha kuukomboa mwili kutoka kwa maradhi na kuurudishia afya na uhai. Uponyaji huu ni haki yako ni mapenzi timilifu ya Mungu kwako na tendo la upatanisho kupitia kwa damu iliyomwagika ya Yesu. Maradhi hayana haki ya kuishi mwilini mwako kama mgeni alivyo na haki kumiliki nyumba ya mtu mtu mwingine. Si haki kwa ugonjwa kukutawala wewe, kuukubali ni kufanya urafiki na adui wa Mungu ambaye amehukumiwa. Yesu Kristo amekukomboa kwa kufufuka kutoka kwa wafu. Ni haki yako kuponywa, kukombolewa na kuwa mshindi. Mungu ameahidi afya kwa kila mtu (Mith. 4:22; 1 Pet. 2:24). 1 Peter 2:24 sio tu ahadi bali ni thibitisho (kamailivyo Math 8:17); inatambua tendo lililokamilika na kuhakikishwa na Yesu. Hakuna yeyote anayefurahia ukamilifu wa Roho na ajuaye ukombozi anayefaa kusumbuka kimwili awe ameshiba au amelala. Yafaa unapoishi duniani usiwe na maumivu yoyote. Huduma ya uponyaji ya Yesu yadhihirisha kwamba ametukomboa kutoka kwa maradhi na ugonjwa. Yesu hakuja tu kuokoa roho zetu bali pia kuponya mwili unaougua. Hivyo basi alimwuliza mtu aliyepindika lipi rahisi kusema, Dhambi zako zimesamehewa au InukaUende? Math 9:5. Huduma ya Kristo ilinuia kuleta ukamilifu wa roho, nafsi na mwili. Mungu siku zote ni mponyaji na ataendelea kuwa mponyaji milele. Uponyaji wako upo. Kumbuka Yesu aliwaponya wote waliomjia wala hakumfukuza mtu yeyote. Hakuna wakati ambapo yesu alisema si mapenzi ya Mungu kumponya mtu au kwamba ilikuwa mapenzi ya Mungu mtu aendelee kuugua. Hakuna ugonjwa unamfunza mtu wala kumsaidia mtu kukua kiroho. Yesu aliwaponya wote waliomjia na hivyo kudhihirisha mapenzi ya Mungu yasiyobadilika ni kuponya kila mgonjwa. Kiini cha Magonjwa Maradhi ni chanzo cha kifo, nacho kifo ni mshahara wa dhambi. Kumbuka hakukuwa na magonjwa hadi Adamu alipotenda dhambi. Hakuna maradhi katika ufalme wa Mungu. Magonjwa yanatokana na dhambi ya asili. Kama dhambi haingekuweko, maradhi nayo hayangekuweko. 167 Elewa kuwa maradhi yanatoka kwa shetani. Jinsi Mungu alivyomtia Yesu wa Nazareti mafuta katika Roho Mtakatifu na jinsi alivyokwenda huku na huko akitenda mema na kuponya wote waliokuwa wameonewa na nguvu za Shetani, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.. Mat 10:38. Tuongeze kuwa udhaifu pia unatoka kwa shetani Wakati uo huo akaja mwanamke mmoja aliyekuwa na pepo mchafu, naye alikuwa amepinda mgongo kwa muda wa miaka kumi na minane, wala alikuwa hawezi kunyoka wima. Yesu alipomwona, akamwita akamwambia, Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako. Yesu alipomwekea mikono Yake, mara akasimama wima akaanza kumtukuza Mungu Luka 13: Yesu alikuwa akifanya mapenzi ya Baba na kwa kufanya hivyo akiharibu kazi za shetani (Ebr. 2:14 na 1 Yohn 3:8). Tazama maandiko uone jinsi ambavyo maradhi yanaelezewa kuwa kazi ya shetani. Tangu siku ile Basi Shetani akatoka mbele za BWANA naye akampiga Ayubu kwa majipu mabaya tangu nyayo za miguu yake hadi utosi wa kichwa. (Ayu 2:7) hadi wakati mkombozi alikuja na kumfungua Je, huyu mwanamke, ambaye ni binti wa Abrahamu, aliyeteswa na Shetani akiwa amemfunga kwa miaka yote hii kumi na minane, hakustahili kufunguliwa kutoka katika kifungo hicho siku ya Sabato? (Luka 13:16), Yesu aliziharibu kazi za shetani Basi kwa kuwa watoto wana nyama na damu, Yeye pia alishiriki katika ubinadamu wao, ili kwa kifo chake, apate kumwangamiza huyo mwenye nguvu za mauti, yaani, Shetani Ebr. 2:14. Tangu mwanzo wetu, shetani amekuwa akishurutisha kizazi chetu kuvuna mazao ya maradhi, maumivu, na kuharibika. Watu wa Mungu mara nyingi hudanganywa na adui hadi kukubali magonjwa kama sehemu yao badala ya kutafuta afya na ukombozi. Upatanisho wa Kristo ulifunika Maradhi Yetu Mojawapo ya sababu za kuja kwa Kristo ilikuwa kuwakomboa watu kutoka katika uongo na utawala wa shetani ikiwemo maradhi ya kiakili na kimwili. Yesu alituokoa kutoka kwa maradhi na dhambi zetu: Lakini alitobolewa kwa ajili ya makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu, adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona Isa 53:5. Utakumbuka kuwa Mungu alimwambia Musa atengeneze nyoka wa shaba kama aina ya Kristo (Hesabu 21:8-9) ili kuwaokoa watu kutoka kwa mauti. Iwapo uponyaji wa mwili haupatikani, kwa nini Wanawaisraeli waliokuwa wakifa walihitajika kumtazama nyoka wa shaba ili waishi (uponyaji wa mwili). Kama ilivyoondolewa laana yao kwa kumtazama nyoka, ndivyo inavyoondolewa laana yetu kwa kumtazama Kristo aliyeinuliwa. Kifo cha Yesu kilitupatia wokovu na uponyaji: akusamehe dhambi zako zote na kuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, na kukuvika taji ya upendo na huruma Zab. 103:3-4. Uponyaji ni dhihirisho la Upatanisho wa Kristo: Mwenyewe alitwaa udhaifu wetu na alichukua magonjwa yetu. Math 8:17. Petro anasema hivi kuhusu kifo cha Yesu: Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake, juu ya mti, ili kwamba,tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tupate kuishi katika haki. Kwa kupigwa kwake, ninyi mmeponywa 1 Pet. 2:24. Kumbuka ushuhuda wa Petro juu ya upako wa Yesu wa uponyaji kakia Matendo 10:38: Jinsi Mungu alivyomtia Yesu wa Nazareti mafuta katika Roho Mtakatifu na jinsi alivyokwenda huku na huko akitenda mema na kuponya wote waliokuwa wameonewa na nguvu za Shetani, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye. Uponyaji kaika Agano Jipya Yesu alihudumia wagonjwa: Yesu akapita katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri Habari Njema za Ufalme wa Mungu, akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi miongoni mwa watu.. Math 4:23. Tafakari yafuatayo: 168 20% ya jumbe zote kwenye Injili ni juu ya uponyaji. Maandiko 41 katika Injili yanazungumzia uponyaji uliofanywa na Yesu Mara 19 Bibilia inaelezea idadi ya watu walioponywa na Yesu. Yesu aliwatuma wanafunzi wake kuponya (Luka 9:1-2 na 10:1, 9). Yesu aliaagiza wanafunzi wake kuponya (Mark 16:15-18). Kwa nini Yesu Aliponya? 1. Kutimiza unabii na kushuhudia Ufalme ujao wa Mungu (Math. 8:16-17) 2. Kuthibitisha yeye alikuwa Masihi (Matendo 2:22-24) 3. Kudhihirisha uwezo wake kusamehe dhambi (Math 9:1-8) 4. Kuonyesha kazi za Mungu (Yoh 9:13-25) 5. Kumtukuza Mungu (Yohn 11:4) 6. Kuwaleta watu kwenye imani (Yoh 20:30-31) 7. Kwa ajili ya huruma na uendo wake kwa watu (Math 20:34) Je Uponyaji ni Kwa Wote? Je wote huponywa? La. Je Yesu alikufa kuokoa wenye dhambi wote? Ndio. Kila mwenye dhambi ana haki ya kuokolewa lakini si wote wanaokoka. Kadhalika na uponyaji wa mwili, kupokea kipawa sio jambo la lazima bali ni hiari ya mtu mhitaji. Kuna watu wengi wagonjwa ambao hawajui wala kuamini kuwa ni haki yao kuponywa. Miili yetu ni Hekalu la Mungu Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu, akaaye ndani yenu, ambaye mmepewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe, kwa maana mmenunuliwa kwa gharama. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu na katika roho zenu ambazo ni mali ya Mungu. 1 Kor. 6: Mwili wako ni jengo takatifu la Mungu, ndio sehemu muhimu sana duniani anapotaka kuishi Mungu. Tunapobatizwa tunawekwa wakfu kwa Mungu na kusudi lake. Baadaye tunaachilia mawazo maovu yaingie na kuishi ndani yetu hata kusababisha maradhi. Lazima tujue kuwa kila wakatimiili yetu ni mali ya Mungu na inatupasa tufanye kila jambo kwa utukufu wake (Warum12:1). Uponyaji na Miujiza Uponyaji wa kimwili ni zaidi ya kurudi uhai katika viungo vinavyougua na kuondoa maumivu. Uponyaji huchukua muda wakati mwingine haraka na mwingine polepole. Ili uponyaji ukamilike, wakati mwingine inabidi kufanyike awamu kadha za maombi. Wakati mwingine muujiza unafanyika kwa haraka.. Wale wanaotafuta uponyaji hutaka muujiza kuponywa mara hiyo papo hapo lakini Mungu aweza kutumia mwelekeo wa uponyaji wa majira kidogo kila siku mpaka kufikia ukamilifu. Ni rahisi kwa mtu kuhifadhi uponyaji wake kuliko kutafuta uponyaji. Pindi imani ya uponyaji ipatikanapo na kanuni zake kueleweka, tusitarajie kuugua. Mungu ali- 169 powatoa Waisraeli kutoka Misri(milioni 5-6) hakuwepo mdhaifu hata mmoja kati yao (Zab ) uponyaji timilifu hudumu kadri tunvyomsongelea Mungu. Uponyaji na Dawa Wengine husema Kama ni mapenzi ya Mungu kuniponya, kuna haja gani kutumia dawa na madaktari Ni kweli kuwa Isaya alimwambia Hezekia achukue matunda ya mtini na kuyaweka kwenye jipu (2 Fal 20:7), lakini pia tunda la mtini halikumponya. Hata hivyo aya ya 1 yatujulisha kuwa Hezekia alikuwa na ugonjwa wa kufisha, aya ya 5 yatuelekeza kuwa Mungu alisema nitakuponya. Kama Yesu alivyochukua udongo akampaka kipofu machoni, twajua kuwa udongo haukuleta uponyaji maana alimwamuru akanawe uso.hakuna kisa kingine ambapo udongo ulitumika kama dawa ya kuponya upofu. Badala yake alichanganya mate na udongo kama tendo la kutii kwa Yule kipofu(yoh 9:6). Kutii kwake ilikuwa ishara ya imani. Kisa cha Naamani (2 Fal 5:1-27) aliyedhani maagizo ya kwenda kujitosa Yordani mara saba (aya ya 10 kwa uponyaji wake) ilikuwa ni kitendo cha kumdunisha/dharau. Sawa na Yule kipofu, wote walitii na kupokea Baraka ya uponyaji. Pia imenakilwa na Timotheo mvinyo kidogo (1 Tim. 5:23) ulipendekezwa kwa ajili ya maumivu ya tumbo. Hivyo basi matumizi ya dawa chini ya maagizo yafaayo ni sawa kwetu. Yafikirie maandiko yafuatayo kuhusu matumizi ya dawa na kuwaona madaktari: 1. hakuna dawa ya kidonda chako, wewe hutapona Yer. 30: Lakini umetumia dawa nyingi bila mafanikio, huwezi kupona. Yer. 46: ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote! Ayu 13:4. 4. Asa alipatwa na ugonjwa kwenye miguu yake. Ingawa ugonjwa wake ulimzidia sana, hata katika kuugua kwake hakutafuta msaada kutoka kwa BWANA bali kwa matabibu tu 2 Nya. 16: Hapo palikuwa na mwanamke aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili. Mwanamke huyu alikuwa ameteseka sana kwa mikono ya matabibu wengi na kutumia kila kitu alichokuwa nacho lakini badala ya kupona hali yake ilizidi kuwa mbaya Mark 5: Mungu amewapa madaktari busara na elimu na kuumba vitu ambavyo hutumiwa kutengeneza madawa ambayo madaktari hutumia kutibu maradhi. Ijapokuwa madaktari wana ujuzi wa kusaidia katika matukio ya ajali, kuzama au dharura ambapo mtu hawezi kujisaidia, yapasa ikumbukwe kujwa Mungu ndiye anayeponya. Kutumia dawa na madaktari sio dhambi na inakubalika na Mungu lakini sio njia ya pekee wala mapenzi timilifu ya Mungu. Kumuona daktari ni muhimu hadi imani ifikie upeo kwa muumini kupokea uponyaji wake kutoka kwa Mungu. Mateso ya Ukombozi? Je maradhi ni mapenzi ya Mungu? La, hasha! Maradhi hayatoki kwa Mungu, huja tu kama majaribu yanavyoruhusiwa kuja kwetu. Mungu anaweza kuruhusu maradhi kuja kama alivofanya kwa Ayubu lakini hatumi maradhi. Iwapo maradhi ni Baraka na mapenzi ya Mungu, basi ni dhambi na kinyume cha mapenzi ya Mungu kuombea uponyaji. Kuna tofauti kati ya (1) ugonjwa na kuugua, na (2)majaribu, mtihani, adhabu, kurudiwa, mateso, na mashaka.mungu anaahidi kuwa tutakumbwa na mashaka, taabu, majaribu, mateso, na usumbufu (Ebr. 11:37-40; 1 Pet. 4:12; Yohn 16:33; Mat 14:22; 2 Kor. 1:6; Zab 34:19; 2 Tim. 3:12 na 4:5) kutakasa nafsi, kukuza utu wa kiroho na uhusiano wetu na Mungu. Hii si sawa na maradhi au udhaifu. 170 Wakati mwingine Mungu hutumia maradhi na ugonjwa kutuelekeza kiroho, lakini hasababishi maradhi haya kutujia wala sio kusudi lake kuyatumia kutukuza sisi kiroho. Hata hivyo kuna uhusiano kati ya dhambi na maradhi, na wakati mwingine Mungu hatatuponya mpaka tuachane na dhambi zetu(luka 5:20 na 7:47-48; Yak. 4:14-16 na Zab 66:18). Tazama aina ya usumbufu uliotajwa katika maandiko yafuatayo. Yote hayaambatani na maradhi (2 Kor. 6:4-5, 11:23-28 na 12:10-11): masaibu mahitaji matatizo viboko kifungo vurugu kazi kukesha uchovu kufunga maumivu ya mwili uchi njaa kiu kuweweseka maradhi kuzomewa mateso mapigano kupigwa mawe kuzama wezi nyikani ndugu bandia uchovu baridi uvumilivu mateso shida za baharini kuteswa na jamaa zako Neno mateso limeandikwa mara 54 katika Agano Jipya na hujumuisha mateso, usumbufu, njaa au hukumu ya mwisho lakini sio maradhi. Neno sumbuka limeandikwa mara 65 katika Agano Jipya ambapo ni mara moja tu ambapo linazungumzia ugonjwa ambao umesababishwa na shambulizi la kishetani sio ugonjwa wa kawaida. Kwa nini basi tusumbuke? Kukuza na kujaribu imani yetu Yak. 1:24 Kubadili uasi na dhambi 1 Kor. 11:30; Yak. 5:13-15 Kujifunza utiifu Ebr. 5:8 Kukuza unyenyekevu 2 Kor. 12:7 (Mwiba wa Paulo) Kumtukuza Mungu 1 Pet. 4:13-14 Tazama tofauti iliyoko hapa: (1) Yak. 5:13, Je, mtu ye yote miongoni mwenu amepatwa na taabu? Basi inampasa aombe., kasha inafuatwa na, (2) Yak. 5:14, Je, kuna ye yote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Basi inampasa awaite wazee wa kanisa wamwombee na kumpaka mafuta kwa Jina la Bwana. Yakobo anaeleza tofauti ya ugonjwa na kupatwa na taabu. Mwiba wa Paulo mwilini haujazungumziwa katika Bibilia nzima isipokuwa kama mfano. Kwengineko katika Bibilia neno mwiba linapotumika tunaona mwiba wenyewe ukitajwa. Katika Hesabu 33:55, Musa aliwaelekeza Wanawaisraeli kabla ya kuingia katika mji wa Kanani, Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wakaao katika nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama miiba kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi. Mwiba huu utakuwa usumbufu katika nchi mtakayoishi- usumbufu wa kila mara. Paulo anaeleza kuwa malaika wa shetani alimtesa. Mwiba wa Paulo haukuwa maradhi. Twaweza kutarajia majaribu na mateso ya kila aina Mungu anapoijaribu imani yetu na kutukuza katika mwendo wetu naye. Lakini hatufai kufikiria kuwa maradhi ni mapenzi ya Mungu au kuyakubali kama chombo cha ukombozi. Yapasa tuwe waangalifu tunapo- 171 muombea mtu aliye majaribuni au kwenye mateso. Iwapo majaribu au mateso yanatekeleza kusudi la Mungu wakati huo nasi tuombe yakome itakuwa tunakwenda kinyume na mapenzi ya Mungu. Ni vigumu kutambua tofauti kati ya majaribu na mateso yatokanayo na yafuatayo: Maisha ya ulimwengu yenye uasi kwa wale wasiomjua Kristo Dhambi na uasi kwale wanaomjua Kristo Laana na athari za vizazi vilivyotangulia Hofu na utovu wa imani kwa wale wanaomjua Kristo Majaribu na Mateso ya wale wanaotembea na Kristo Kuna tofauti za ndani ambazo zaweza kujulikana tu na wale walio na kipawa cha kupambanua roho au ufunuo. Kadri mnapoomba kwa Baba juu ya matukio ya maisha yako, Mungu atatoa jawabu na kubainisha ukweli ulipo. Ponya Roho Kwanza Mnamo 1976, Francis MacNutt aliandika kitabu kiitwacho Healing ambamo aliorodhesha aina nne za uponyaji: (1) Uponyaji wa Roho, (2) Uponyaji wa hisia na mioyo iliyovunjika, (3) uponyaji kutokana na athari za giza, na (4) uponyaji wa miili yetu. Watu wengi huja na hitaji la kuponywa mwili kwanza kabla ya kutafuta uponyaji wa roho. Mungu anhusika na uponyaji wa roho(toba) na hufurahia uponyaji wa roho ndiposa mwili ufuatie. Kwanza tunatakasa chombo cha ndani(roho na nafsi) ndipo kuwe na nuru itakayoruhusu uhai wa Yesu kuingia mwilini kwetu. Pingamizi kubwa ya uponyaji ni pepo mchafu. Kuna uhusiano unaobainika kati ya dhambi na ugonjwa na mara nyingi Bwana hatuponyi maradhi mpaka tutubu (Zab 66:18, Luka 5:20; Luka 7:47-48; Yak. 4:14-16;). Mungu hakuahidi kuharibu kazi za shetani iwapo tunazingatia matendo ya giza. Dhambi ambayo haijaungamwa huzuia rehema za Mungu kutufikia. Kumbuka, Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali ye yote aziungamaye na kuziacha hupata rehema. Mith. 28:13. Ugonjwa ni roho ya maradhi. Ukiponywa ndani ya nafsi yako hata mwili wako utapona. Shida yote iko inasababishwa na usafi au uchafu wa roho. Uponyaji hugusa maeneo matatu: roho, nafsi na mwili. Jua kuwa mwili wako huathiriwa na roho yako ( Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo 3 John 2). Huwezi kupokea uponyaji wa mwili kabla ya kupokea uponyaji wa roho. Uhusiano kati ya Maradhi na Dhambi Tazama hatua ya dhambi na maradhi katika maandiko yafuatayo. 3akusamehe dhambi zako zote na kuponya magonjwa yako yote,.(zab 103:3) and naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako kama vile roho yako ifanikiwavyo. (3 Yohn 2). Kuna uhusiano kati ya maradhi na dhambi. Maradhi yote ni matokeo ya: a) kutengwa na Mungu (uasi) b) kutengwa kwa nafsi (kujichukia) c) kutengwa na wengine (kutosamehe, hasira, majeraha) 172 Utafiti waonyesha kuwa 80% ya magonjwa yanaathiri akili, yaani hutokana na mawazo, hisia na matatizo katika roho zetu wala sio magonjwa yenyewe. Mwili unaitikia hali iliyoko kwenye nafsi na roho. Adui huleta yafuatayao: kujichukia kutosamehe hofu hukumu chuki kiwewe kujikataa machungu wasiwasi hofu ya kukataliwa hasira kujisukuma kujikana maudhi kujipenda kujihukumu farakano kwenye jamii kujidunisha miili yetu nayo inaitikia na chembe za damu zinaanza kuugua. Chembe zinazozuia maradhi zinaharibika na hivyo basi wewe unaanza kuwa mgonjwa. Unapohisi au kusema mambo yaliyo hapo juu, roho ya kuugua inapata kibali cha kuingia ndani yako. Roho hii inaanza kuumiza mwili mpaka uishie kuwa na maradhi yafuatayo: mizio ugonjwa moyo, mshipa kasi ya damu kuvunda kwa damu Kuvunjika mifupa kuzimia kifafa kisukari saratani Utengano unapoponywa (yaani kujichukia, kutosamehe, kujikataa) chembe chembe za damu zinazopigana na maradhi huanza kufanya kazi kama zilivyokusudiwa. Ili kujifunza zaidi, tazama: Henry W. Wright A More Excellent Way, Be in Health, ISBN Uponyaji Kanisani Kuna aina mbili za uponyaji kanisani: (1) huduma inayofanywa na wachache wenye vipawa na (2) uponyaji unaofanywa kanisa zima kwenye ibada za uponyaji au vipindi vya huduma baada ya ibada. Huduma ya Uponyaji Fuata hatua zifuatazo kuanzisha huduma ya uponyaji kanisani: 1. Mfano kuwa na vipindi na kanuni za uponyaji kwa kuzoea kuhubiri na kufundisha juu ya uponyaji ili uongozi na washirika wawe na uzoefu wa kuponya na kukuza imani katika huduma hii ya uponyaji. 2. Fundisha na kutia hima ushirika kuhusika na uponyaji katika mafundisho na mahubiri ukitumia wahuduma waalikwa wenye vipawa vya kufundisha na kutoa mifano ya uponyaji. Tambua walio na vipaji vya uponyaji na wale wanaotamani kujifunza, kuponya na kuendeleza vipaji vyao. 4. Funza na kuwapa vifaa vikundi vya huduma chini ya viongozi muafaka. 5. Tuma vikundi vya huduma kwenye maeneo kila juma ili waweze kuimarisha huduma yao. 6. Wape wahuduma nafasi ya kukuza vipaji na uwajibikaji. 7. Rudia hatua hizi na vikundi vipya vinapojiunga na huduma ya uponyaji Tazama kitabu: How to Have a Healing Ministry in Any Church, na C. Peter Wagner (kinapatikana kupitia Amazon.com) Ibada za Uponyaji Kanisani Kuna upako mkuu ndani ya ibada zilizopangwa maalum kwa ajili ya uponyaji kuliko katika maombi ya mtu binafsi nyumbani. Kuna aina sita ya matukio ambamo Mungu huponya kwenye ibada hizi: 1. kwenye ibada ya sifa na kuabudu 2. watu wanaposhuhudia uponyaji kwenye mikutano au filamu za video 3. watafutaji wanapopumzika katika roho 4. katika maneno ya utambuzi 5. kiongozi anapoombea kundi zima 6. watafutaji wanapoombewa na kundi la waombezi wa huduma ya ukombozi Tambua matukio matatu ya hapo juu ni matendo ya neema ya Mungu pasipo nguvu za mwanadamu kuhusika. Uponyaji huu ni bora kwa kuwa Mungu pekee hupokea utukufu. Tukio la mwisho peke yake ndilo linalohusisha kuwekewa mikono. Mungu huitikia sifa, ibada na imani. Kila ibada ya uponyaji yapasa kuanza na kipindi cha sifa na ibada. Iwapo kundi halijafundishwa juu ya huduma ya uponyaji, mafundisho ya maandiko yapaswa kufanywa kabla ya huduma kuanza ili watu wafahamu haki zao za uponyaji kutokana na upatanisho wa Kristo. Pia yafaa kujenga imani kwenye maandiko na mifano ya uponyaji na namna ambavyo Mungu huponya. Shuhuda na filamu za video zaweza kutumika iwapo zinapatikana. Kabla ya mkutano mchungaji aamue iwapo atafanya maombi yote au atasaidiwa na kundi la waombezi. Hata hivyo ieleweke kuwa mchungaji anapofanya maombi yote anaweza kuzuia wengine walio na kipaji cha uponyaji kukitumia. Maneno ya Utambuzi Neno la utambuzi ni ufunuo unaotolewa na Roho Mtakatifu. Paulo alipokeamaneno haya ya utambuzi kupitia ufunuo (1 Kor. 2:12-13). Roho Mtakatifu hutoa ufunuo kuhusu h
Search Related
We Need Your Support
Thank you for visiting our website and your interest in our free products and services. We are nonprofit website to share and download documents. To the running of this website, we need your help to support us.

Thanks to everyone for your continued support.

No, Thanks